Monday, October 1, 2012

STEVEN GERRARD: KUNYAKUA UBINGWA WA LIGI KUU NIKIWA LIVERPOOL, HUO UTAKUWA MUUJIZA

Steven Gerrard

Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard amesema kuwa itakuwa ni muujiza kwa klabu yake kushinda taji la ligi kuu kabla ya yeye kustaafu soka.
Liverpool ambao walishinda kwa mara ya mwisho taji hilo mwaka 1990 wanashikilia nafasi ya 14 katika msimamo wa ligi baada ya kuanza vibaya msimu huu.
"Itakuwa muujiza kama tutashinda taji la ligi kabla sijastaafu soka" Steven Gerrard,32, aliliambia gazeti la The Sunday Times la Uingereza."Nasema hivyo kutokana na umri wangu na hali halisi ya wapinzani wetu.Ligim imekuwa ngumu sana kushinda kwa sasa.
Gerard anaamini kwamba ujio wa timu kama Manchester City ,ambao walishinda taji hilo msimu uliopita inafanya kuona ndito yake kama kitu ambacho hakiwezekani kutimia.
Alisema, ''Sio tu [Manchester] United na Arsenal kwasasa lakini pia [Manchester] City, Chelsea na Tottenham. Newcastle wanakuja juu pia.
Tulishika nafasi ya nane msimu uliopita.Kama msimu huu mambo yakienda vizuri, tukawa na bahati nzuri, tukajitahidi, tuna asilimia 50 kwa 50 ya kumaliza katika nafasi nne za juu.Hilo linawezekana."
Gerrard ambaye alizaliwa Merseyside, alijiunga na chuo cha soka cha Liverpool akiwa na umri wa miaka tisa na alisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo mwaka 1997.

No comments:

Post a Comment