Friday, October 5, 2012

MAGAZETI YOTE YA LEO
IJUMAA OKTOBA 05, 2012

BOFYA HAPA KUSOMA MAGAZETI YOTE YA LEO...STORI ZA MBELE MAGAZETI YA HABARI, MICHEZO, BURUDANI, UDAKU
MECHI YA SIMBA NA YANGA YAINGIZA TSHS 390...KLABU ZAAMBULIA MIL 93

MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom baina ya watani wa jadi Yanga na Simba iliyochezwa jana (Oktoba 3 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 imeingiza Sh. 390,568,000, lakini makato makubwa kupitiliza katika uwanja huo yameendelea kutozinufaisha klabu.
 

Katika mgawo, Yanga na Simba kila moja zimepata Sh.milioni 93 ambazo jumla yake inakuwa ni Sh. milioni 186 wakati makato ni mengi zaidi kiasi ambacho klabu hizo mbili zinapata. Jumla ya makato ni Sh. milioni 203. 


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, watazamaji 50,455 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kuanzia saa 1 usiku kwa viingilio vya Sh. 5,000, Sh. 7,000, Sh. 10,000, Sh. 15,000, Sh. 20,000 na Sh. 30,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa Sh. 93,345,549.15 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni Sh. 59,578,169.49.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 240,000, kamishna wa mechi sh. 250,000, waamuzi sh. 591,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.

Umeme sh. 750,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 5,860,000 wakati tiketi ni sh. 7,327,000. Gharama za mchezo sh. 31,115,183.05, uwanja sh. 31,115,183.05, Kamati ya Ligi sh. 31,115,183.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,669,109.83 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,446,073.22.

Wakati huo huo, mechi ya ligi hiyo kati ya African Lyon na Toto Africans iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex na kushuhudiwa na washabiki tisa kwa kiingilio cha sh. 3,000 imeingiza sh. 27,000.

Mgawo wa mechi hiyo ulikuwa VAT sh. 4,118.6 wakati kila timu ilipata sh. 6,864.3. Uwanja sh. 2,288.1, gharama za mchezo sh. 2,288.1, Kamati ya Ligi sh. 2,288.1, FDF sh. 1,372.8 na DRFA sh. 915.2

Katika mechi hiyo, kiungo Amri Kiemba aliifungia Simba goli lao katika dakika 4 kufuatia krosi ya Mwinyi Kazimoto kabla ya Yanga kusawazisha kupitia kwa straika Said Bahanunzi katika dakika ya 65 kwa penalti iliyotolewa na Mathew Akrama baada ya 
beki wa Simba, Paul Ngalema kushika mpira ndani ya 18 wakati akijaribu kuokoa mpira wa kona kwa kichwa.

Wednesday, October 3, 2012

NAHODHA WA BARCELONA CARLES PUYOL AUMIA VIBAYA MKONO...HATOWEZA KUCHEZA MECHI YA EL-CLASSICO DHIDI YA REAL MADRID ITAKAYOFANYIKA JUMAPILI
Carles Puyol akipata huduma ya kwanza baada ya kuumia wakati wa mechi yao ya Kundi G la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Luz mjini Lisbon, jana Oktoba 2, 2012. (Picha: REUTERS)

Carles Puyol akitolewa kwa machela kuwahishwa hospitali baada ya kuanguka vibaya na kutenguka mkono wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Benfica kwenye Uwanja wa Luz mjini Lisbon jana usiku, Oktoba 2, 2012. (Picha: REUTERS)

Kocha wa Barca, Tito Vilanova (kulia) akionekana kusikitika wakati nahodha wake Carles Puyol akitolewa kwa machela baada ya kuanguka vibaya na kutenguka kiwiko cha mkono wakati akiwania mpira wa kichwa katika mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Benfica kwenye Uwanja wa Luz mjini Lisbon jana usiku, Oktoba 2, 2012. (Picha: REUTERS)
LISBON, Ureno
Beki wa kati wa Barcelona, Carles Puyol alikimbiziwa hospitali baada ya kutengua kiwiko cha mkono wake wa kushoto katika ushindi wao wa ugenini wa 2-0 kwenye mechi ya Kundi G la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Benfica jana na hivyo atakosa mechi ya 'El Clasico' watakayocheza Jumapili dhidi ya Real Madrid kwenye Uwanja wa Nou Camp.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania, akicheza katika mechi yake ya kwanza tangu apone jeraha la goti, aliangukia mkono aliporuka kuufuata mpira wa kona.

Nahodha huyo wa Barca mwenye miaka 34 alitolewa katika machela huku akionekana kuwa na maumivu makali katika dakika ya 78 na nafasi yake ikachukuliwa na Alex Song wakati wenzake wakionekana kustushwa na tukio hilo.

"Tunasubiri taarifa zaidi lakini ni wazi kwamba atakosa mechi ya 'Clasico'," kocha wa Barca, Tito Vilanova aliwaambia waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mechi hiyo.

Jeraha limekuja katika wakati mgumu kwa Barcelona ambayo pia inamkosa pacha wa Puyol katika nafasi ya ulinzi wa kati, Gerard Pique ambaye pia ni majeruhi.

Barca ilishinda mjini Lisbon, ukiwa ni ushindi wao wa pili katika mechi zao mbili za Kundi G, shukrani zikiwaendea wafungaji Alexis Sanchez na Cesc Fabregas.

"Sasa tunapaswa kusahahu kuhusu Ligi ya Klabu Bingwa na kuangalia namna ya kuitumia vyema fursa ya kufanya vizuri tukiwa nyumbani (Jumapili)," alisema beki wa pembeni wa Barca, Dani Alves, ambaye alionekana kustushwa na jeraha alilopata Puyol.

"Tunajua itakuwa mechi ngumu."

Barcelona wako kileleni mwa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania kwa pointi nane zaidi ya mahasimu wao wa jadi, Real Madrid ikiwa ni baada ya kila timu kucheza mechi sita.
MAGAZETI YOTE YA LEO
JUMATANO OKTOBA 03, 2012



BOFYA HAPA KUSOMA MAGAZETI YOTE YA LEO...STORI ZA MBELE MAGAZETI YA HABARI, MICHEZO, BURUDANI, UDAKU
MSANII DIAMOND ASAINI MKATABA NA KAMPUNI


Msanii Diamond Platnumz (wa pili kulia) akibadilishana mkataba wa kusimamiwa na mkurugenzi wa kampuni ya I-View Studios, Raqey Mohammed (kushoto) baada ya kusaini. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, mwanasheria wa I-View Dr. Peter Aringo na mkurugenzi wa One Touch Solutions, Petter Mwendapole.

MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz ameingia mkataba na kampuni ya I-View Studios ya ili wasimamie kazi zote kwa muda wa miaka miwili.

Mkurugenzi wa kampuni ya uwakala ya One Touch Solution ya mjini Dar es Salaam, Petter Mwendapole alisema I-View itasimamia mikataba yote ya kazi zote za msanii huyo na yeyote atakayetaka kufanya kazi na Diamond kwa sasa itabidi awasiliane kampuni hiyo.


"Diamond ameamua kufanya kazi zake kimataifa. Ameingia mkataba na I-View ambao watakuwa wakisimamia maonyesho, matangazo, nyimbo kwenye simu, nguo na kila kitu kinachohusiana na yeye kinapaswa kupitia kwao," alisema.


Mwendapole alisema pamoja na maonyesho, kampuni hiyo pia itawajibika katika muonekano mpya wa msanii huyo anayetamba ndani na nje ya Tanzania na kwamba kampuni ya uwakala ya One Touch Solutions ndiyo watakaokuwa wasemaji wa msanii huyo.


Diamond kwa upande wake alisema anataka kufungua ukurasa upya katika tasnia ya muziki nchini na anaamini utasaidia katika kumfanya aongeze nguvu zaidi katika kutunga na kutengeneza nyimbo bora.


“Hii yote ni kuhakikisha nafanya kazi zangu kwa ufanisi badala ya kujirundikia mambo mengi, kuna watu walikuwa wakinitafuta wanashindwa kunipata lakini sasa watakuwa wanafahamu ofisi ziko wapi na wanawasiliana na menejimenti, watu wa habari watakuwa na mtu wa kuwasiliana naye moja kwa moja hata kama sipatikani,” alisema.


Diamond anatarajia kutoa wimbo wake mpya ambao pia utarekodiwa na kampuni ya I-View. Tayari usaili umeshafanyika kwa ajili ya wale ambao wataonekana kwenye video ya wimbo huo.


I-View mbali na kazi kupiga picha, lakini pia inatengeneza matangazo mbalimbali ya TV, Radio, mabango, ubunifu wa kazi mbalimbali za sanaa.
MATOKEO YA MECHI ZA JANA ZA LIGI KLABU BINGWA ULAYA


HIZI NDIZO PICHA ZA AJALI YA JANA ILIYOTOKEA JANA MBEYA











Tuesday, October 2, 2012

ZLATAN IBROHIMOVICH: MESSI HASTAHILI KUWA MCHEZAJI BORA WA DUNIA KWA MAKA HUU

Ibrahimovich akimtazama Messi enzi hizo wakiwa wote Barcelona

Ibrahimovich akifurahia ushindi pamoja na Messi enzi hizo wakiwa wote Barcelona
Mchezaji wa zamani wa Barcelona na Intermilan Zlatan Ibrahimovich amefunguka na kusema kuwa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi hastahili kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa dunia mwaka huu kwa sababu msimu uliopita ameshinda kikombe kimoja tu kidogo, mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona Zlatan Ibrahimovic amesema leo Jumanne.

"Messi amekuwa na msimu mzuri binafsi lakini hajashinda kitu chochote kikubwa na tayari ameshashinda Ballon d'Or mara 3," Mshambuliaji wa Pars Saint Germain Ibrahimovic, ambaye alicheza na Messi katika msimu wa 2009/10, aliiambia Eurosport jumanne hii.


"Inategemea aidha unampa mtu zawadi kwa kazi yake binafsi ay yenye mkusanyiko. Xavi bado anacheza katika kiwango cha juu, Iniesta pia alikuwa na msimu mzuri, wameshinda Euro wakati Messi ameshinda kikombe kidogo cha mfalme . Messi ameshahsinda Ballon D'Or mara 3 nafikiri msimu huu hastahili na muda huu nafikiri ni sahihi akishinda mtu mwingine."


Tuzo ya Ballon d'Or  itatolewa mwezi January tarehe 7 mwakani.

JOSE MOURINHO: NAYACHUKIA MAISHA YANGU YA KIJAMII..WATU SASA WANANIDHIHAKI




Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho amesema kuwa umaarufu na kujulikana kunakokuja kupitia kufundisha soka ni mgumu sana kuubeba.
Meneja huyo wa Real Madrid akiongea na CNN,alisema mtoto wake mwenye umri wa miaka 12 amekashifiwa na hiyo inafanya kuwa ngumu kuishi maisha ya kawaida.
"Kama ningeweza kuwa kocha, kocha wa soka, kwa muda huu nikaondoka klabuni baada ya mechi na kuzima mwanga wote na kuwa mtu mpya ambaye hakuna mtu anayemjua, nigefanya kazi hiyo vizuri kwa raha," aliambia CNN.

"Kwasababu nayachukia maisha yangu ya kawaida. Sipendi maisha ya ustaa. Nachukizwa sana na kushindwa kuishi maisha ya kawaida, kama baba ambaye anaenda na mwanae wa kiume kuangalia soka na kuwa pale na wababa wengine 20 tunaangalia mchezo huo.

"Nipo kwenye mechi ya soka ya watoto wa miaka 10-12 na ninatakiwa kuwepo pale, watu wanakuja na kuanza kuomba kupiga nao picha, washabiki wanakuja kwa kutaka kupata saini,Wengine wanakuja kunitukana tu, wengine huenda golini kwenye lango analodaka mwanangu mwenye miaka 12 na kumtukana mwanangu."  
Source:The Independent
BASI LA DAR EXPRESS LILILOKUWA LIKITOKEA ARUSHA KWENDA DAR LATEKETEA KWA MOTO
Basi hilo likiteketea kwa moto
























Habari zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema watu 65 wamenusurika kufa eneo la Segera Mkoani Tanga baada ya basi la Dar Express lililokuwa likitokea Arusha kwenda Dar Es Salaam kuteketezwa na Moto. Picha kwa Hisani ya Jamii Forums
UFAFANUZI WA WATOTO WA STEVEN WASSIRA JUU YA WAO KUJIUNGA CHADEMA
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbrod Slaa akiwakabidhi kadi za Chama Esther Wasira na Lilian Wasira mara baada ya kujiunga na chama hicho
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
UFAFANUZI KUHUSU SISI KUJIUNGA NA CHADEMA NA MALUMBANO KUHUSU MAJINA YETU  Tarehe 30/09/2012 mimi Esther Wasira na dada yangu Lilian Wasira tulijiunga na CHADEMA na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Dr Willibrod Slaa. Tulielezea kwa kirefu sababu za sisi kujiunga CHADEMA na tukasisitiza kuwa tumeridhika kuwa CHADEMA ni chama chenye dhamira safi ya kuiongoza Tanzania na kwamba ni chama kinacholeta matumaini mapya ya kuijenga Tanzania mpya yenye neema. Waandishi wa habari walijaribu sana kutudodosa kujua tuna uhusiano gani na Waziri Steven Wasira. Tulielezea wazi kuwa mahusiano yetu ya kifamilia hayahusiki na sababu na dhamira yetu ya kujiunga CHADEMA. Hata hivyo tulielezea kuwa Waziri Steven Wasira ni baba yetu mdogo ambaye alinyang'anyana ziwa na baba yetu mzazi, wakili George Wasira. Tulidhani hiyo ilitosha na lisingekuwa swala tena la kujadili na badala yake hoja ya kujadiliwa ingeweza kuwa sababu tulizozieleza za kujiunga CHADEMA. Tunasikitishwa sana na malumbano yaliyofuata baada ya hapo kuhusu kama sisi ni watoto wa Wasira au la. Kama tulivyoeleza, tumejiunga CHADEMA kwa sababu tulizozieleza hapo awali na wala si kwa sababu nyingine yeyote. Hatujajiunga CHADEMA kumdhalilisha mtu, kumfedhehesha mtu au kukipatia umaarufu CHADEMA kwa vile tu tunatumia jina la Wasira. CHADEMA ni chama cha siasa tena chenye wanachama na wafuasi wengi Tanzania hivyo si kashfa bali ni fahari kubwa mtu kujiunga CHADEMA na tena ni ushahidi wa mtu kujitambua. Pia CHADEMA ni Chama maarufu sana Tanzania kwa sasa hata pengine ni maarufu kuliko CCM hivyo hakihitaji kujipatia umaarufu kwa mgongo wetu. Sisi tunawaheshimu sana wazee wetu na tutaendelea kuwaheshimu ila linapokuja swala la chama cha kujiunga linabaki kuwa hiari yetu kwa kuzingatia sera za chama na uwezo wa chama husika katika kujenga Tanzania tunayoitaka na hilo ndilo lililotupeleka CHADEMA. Na hii ni haki yetu ya msingi kabisa inayolindwa na Katiba ya nchi hii chini ya ibara ya 20(1). Ikumbukwe kuwa mmoja wa Waanzilishi wa CHADEMA ni Mzee Wasira. Dhamira ya kuanzisha CHADEMA ilikuwa ni kushika dola na hili ndilo CHADEMA imekuwa siku zote inajaribu kuwashawishi Watanzania kuwa sasa wamekomaa na wanastahili kuchukua dola. Kwa vile kuchukua dola ilikuwa ndio ndoto ya baba yetu mzazi Mwanzilishi wa CHADEMA, sisi kama watoto tumejiunga na M4C ya CHADEMA ili tuweze kutimiza ndoto ya baba yetu kuwa CHADEMA siku moja ichukue jukumu la kuiongoza Tanzania.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na: 
Lilian Wasira 0719 604156 
Esther Wasira 0655 048797

MOURINHO: NITARUDI UINGEREZA KUFUNDISHA

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho
Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho amesema atarudi kufundisha soka la nchini Uingereza wakati atakapomaliza mkataba wake na Real Madrid lakini mreno huyo amesema kuwa ana furaha kuwepo Bernabeu.

Wakati kocha huyo wa zamani wa Chelsea akiwa na mkataba na Real Madrid hadi 2016, anadhani kuwa kazi yake ijayo itakuwa ni kurejea katika ligi kuu ya Premier.
''Nimesema wazi kuwa, kwa sababu nyingi, baada ya hili hatua ijayo itakuwa ni Uingereza'' Mourinho mwenye miaka 46 aliiambia CNN.

''Ni lini? sijui, sifahamu.Nina furaha kwa wakati huu kuwa meneja wa klabu bora duniani''.
Mourinho alijiunga Real Madrid akitokea Inter Milan mwaka 2010 baada ya kuipa taji la tatu la Ligi Klabu Bingwa Ulaya timu hiyo ya Italia
TIMU YA ANZHI MAKHACHKALA ANAYOCHEZA SAMUEL ETO'O SASA YAMFUKUZIA KAKA WA MADRID

Ricardo Kaka wa Real Madrid
MOSCOW, UrusiWakala wa Urusi, Shumi Babaev amethibitisha kwamba klabu tajiri ya Anzhi inayoshiriki Ligi Kuu ya Urusi inajiandaa kumtwaa Kaka na kumsajili wakati wa dirisha dogo la usajili wa Januari.

"Anzhi imefikiria kumtwaa Kaka kwa muda mrefu, hata hivyo, yeye si aina ya wachezaji ambao wanaweza kusajiliwa kirahisi. Tunaweza kuzungumzia ujio wake kwa uhakika wakati wa kipindi cha soko la usajili," amesema Babaev.

Kaka alicheza jana wakati Real Madrid ilipocheza dhidi ya Deportivo Coruna katika La Liga, Ligi Kuu ya Hispania ambayo walishinda 5-1.

Hivi sasa, Anzhi ambayo tayari ina "majembe" kadhaa kikosini kama Eto'o, Christopher Samba na Lassana Diara, ndiyo inayoongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya Urusi na kuwapiku vigogo CSKA Moscow, Lokomotov na Zenit St. Petersburg.
MELI MPYA YA AZAM YAWASILI NCHINI...INA UWEZO WA KUBEBA ABIRIA 1000 NA MAGARI 200



Ndg Said Bakhresa (mwenye nguo nyeusi kushoto) akikagua mazingira ya Meli hiyo baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar


Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar.  
Kampuni ya Azam Marine inayomiliki boti ziendazo kasi hapa nchini, leo imeingiza meli mpya na ya kisasa itakayochukua zaiidi ya abiria 1500 na magari 200. Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Marine, Bw. Hussein Mohammed Saidi, amesema leo mjini Zanzibar kuwa meli hiyo ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, zanzibar na Pemba itatoza nauli nafuu kwa abiria wake. 

Amesema meli hiyo ambayo inatarajiwa kuanza safari zake mara baada ya kukamilisha taratibu za mamlaka mbalimbali. Meli hiyo inayoitwa AZAM SEALINKI ni ya kisasa katika ukanda huu wa Mwambao wa nchi za Kusini na Pembe ya Afrika. Bw. Hussein amesema Meli hiyo ambayo imetengenezwa nchini Ugiriki na inatayarishiwa eneo maalumu litakalotumika kwa kupakia na kushusha abiria na mizigo yakiwemo magari. Amesema meli hiyo itasafiri kwa muda wa saa tatu kutoka Dar es salaam na Zanzibar na saa 4 kutoka Zanzibar na Pemba ama saa 7 kutoka dar es salaam na Pemba. 

Amesema pamoja na kuwasili kwa Meli hiyo, Kampuni ya Azam pia inatarajia kuleta meli nyingine ya abiiria inayojulikana kama Kilimanjaro namba 4. Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Visiwa vya zanzibar wamepongeza ujio wa meli hiyo lakini wakaitaka serikali kuendelea kudhibiti uingizwaji wa meli chakavu na kukuu ili kuepuka uwezekano wa kutokea ajali za mara kwa mara. 
Bwana Rajabu Khamisi mkazi wa Pemba na Bi. Rehema Omari wa mjini Zanzibar, wamesema kuna haja ya Serikali kusimamia ukomo wa nauli ili kila mwananchi aweze kusafiri kutoka sehemu moja na nyingine kwani wamesema vipato havilingani.
SUMAYE APATA PIGO URAIS 2015

Frederick Sumaye
NDOTO za Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye za kuwania Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu ujao, zimeingia doa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kupitia Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara. Sumaye ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo la Hanang kwa kipindi kirefu hadi mwaka 2005, ameshindwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk Mary Nagu ambaye amegeuka kuwa mmoja wa hasimu wake wa kisiasa katika siku za karibuni, mbali ya kuwa na mahusiano mazuri kwa miaka mingi.

 Taarifa za Sumaye kushindwa zilianza kuvuja mapema hata kabla ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo saa 10:00 alfajiri jana, kwani baadhi ya wapambe wake walilazimika kuondoka katika ukumbi uliokuwa ukifanyika uchaguzi huo. Msimamizi wa uchaguzi huo ulianza kufanyika juzi asuhubi, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo akitangaza matokeo hayo alisema Sumaye alipata kura 481 huku Dk Nagu akiibuka mshindi kwa kupata kura 648. 

Mgombea mwingine, aliyekuwa anawania nafasi hiyo, Leonce Marmo Bura alitangaza kujitoa mapema ili apate fursa ya kugombea nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambao alishinda. Dk Nagu tangu awali alionekana kuungwa mkono na wajumbe wengi wa mkutano huo hali ambayo ilimfanya wakati wa kujieleza asiulizwe maswali huku mwenzake Sumaye akibanwa kwa maswali mengi. 

Hata hivyo, uhodari za Sumaye, kujibu maswali hayo kwa kiasi fulani ulionekana kutaka kubadili hali ya upepo katika mkutano huo, lakini wakati wa kupiga kura nguvu ya Waziri Dk Nagu ilionekana kurejea upya. Mvutano kati ya Sumaye na Nagu ulianza kuonekana hivi karibuni baada ya kikao cha kamati ya siasa ya Wilaya kilichofanyika Septemba 2, mwaka huu kupitisha jina la Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Leonsi Marmo huku la Nagu likiondolewa kufuatia kudaiwa kuwa na majukumu mengi ya kikazi ikiwamo Ubunge na Uwaziri. Hata hivyo, Nagu alikata rufaa katika Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Manyara ambayo ilirejesha jina lake. 

Kushindwa kwa Sumaye kupata nafasi hiyo kunaonyesha ni kikwazo kipya kwake kama ataamua kuwania Urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa mara nyingine. Sumaye ambaye amekuwa Waziri Mkuu katika utawala wote wa Serikali ya awamu ya tatu ya Rais Benjamin Mkapa aliwania Urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, akishindana na Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela, Dk Abdallah Kigoda na Profesa Mark Mwandosya. 

Hata hivyo, pamoja na kwamba hajaweka wazi kuwa atagombea tena katika uchaguzi wa mwaka 2015, lakini watu walio karibu na mwanasiasa huyo wamekuwa wakieleza kuwa anajiandaa kugombea tena nafasi hiyo. Juzi wakati akijieleza mbele ya wajumbe wa mkutano huo, Sumaye alionekana kushangazwa na hatua ya Dk Nagu kugombea nafasi hiyo, hali akijua kuwa yeye ni Waziri na hivyo kwa utaratibu ndani ya CCM ni mjumbe moja kwa moja wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).
 Kwa upande wa Dk Nagu ambaye aliachiwa kugombea ubunge wa jimbo hilo na Sumaye mwaka 2005, katika siku za karibuni amekuwa akitamba kuwa ni Simba jike, alitumia dakika tatu za kujieleza kukanusha uvumi kuwa ametumwa na makundi mengine ndani ya CCM ili kumzuia Sumaye asiwe Mjumbe wa NEC ikiwa ni harakati za kugombea Urais mwaka 2015. 
Chanzo: Mwananchi
MAGAZETI YOTE YA LEO
JUMANNE OKTOBA 02, 2012

BOFYA HAPA KUSOMA MAGAZETI YOTE YA LEO...STORI ZA MBELE MAGAZETI YA HABARI, MICHEZO, BURUDANI, UDAKU

Monday, October 1, 2012

RATIBA YA MECHI ZA LIGI KLABU BINGWA ULAYA (UEFA CHAMPIONS LEAGUE) WIKI HII


KESHO, Jumanne
Kundi E
    Juventus         v Shakhtar Donetsk       (saa 3:45) usiku
    Nordsjaelland    v Chelsea                     (saa 3:45) usiku

Kundi F

    Valencia      v Lille                                 (saa 3:45) usiku
    BATE Borisov  v  Bayern Munich           (saa 3:45) usiku

Kundi G
    Benfica        v Barcelona                        (saa 3:45) usiku
    Spartak Moscow v Celtic                        (saa 1:00) usiku
   
Kundi H

    CFR Cluj       v Manchester United          (saa 3:45) usiku
    Galatasaray    v Braga                            (saa 3:45) usiku

--------------------------------------------------------------------------------

KESHOKUTWA, Jumatano

Kundi A

    Dynamo Kiev v Dinamo Zagreb               (saa 3:45) usiku
    Porto       v Paris St Germain                   (saa 3:45) usiku

Kundi B

    Schalke 04 v Montpellier HSC                  (saa 3:45) usiku
    Arsenal    v Olympiakos Piraeus               (saa 3:45) usiku

Kundi C

    Anderlecht          v Malaga                       (saa 3:45) usiku
    Zenit St Petersburg v AC Milan                (saa 1:00) usiku

Kundi D

    Manchester City   v Borussia Dortmund   (saa 3:45) usiku 
    Ajax Amsterdam    v Real Madrid             (saa 3:45) usiku