Friday, September 28, 2012

AJILI YA NDEGE YAUA WATU 19....YASHIKA MOTO NA KUTEKETEA...NI BAADA TU YA KUANZA KURUKA

Ndege hiyo ikiteketea kwa motoKathmandu, Nepal (CNN) 
Kumetokea ajali mbaya ya ndege nchini Nepal pale ndege moja ilipokamata moto na kuwaka papo hapo na kusababisha watu wote 19 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo kupoteza maisha ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kuanza kupaa katika mji mkuu wa Kathmandu.Ndani ya ndege hiyo mlikuwa na wasafiri 16 na wafanyakazi wa ndege watatu.Kati ya waliofariki dunia abiria 7 ni raia wa Uingereza, 5 raia wa China alisema Sameer Neupane ambaye ni afisa.Wengine waliofariki ni abiria wanne na wafanyakazi wa ndege hiyo wote wakiwa ni raia wa Nepal.Aidha, maofisa wanachunguza chanzo cha ajali hiyo kwa kufuatilia picha za ndege hiyo tangu ilipoanza kuruka
Chanzo: www.cnn.com

No comments:

Post a Comment