Saturday, September 29, 2012

ANTON FERDINAND:"MIMI SIO MUONGO!".........AKERWA NA WATU WANAOMTUHUMU
Anton Ferdinand
Hatimaye mchezaji Anton Ferdinand amevunja ukimya juu ya John Terry akisema,Mimi siyo Muongo.
Beki huyo wa timu ya QPR alisema hayo kwenye Twitter mara baada ya nahodha wa Chelsea John Terry kukutwa na hatia ya ubaguzi wa rangi na chama cha soka cha Uingereza FA. Ferdinand aliandika ''Watu wanapaswa kusoma uhalisia kabla ya kunitumia tweets za kipuuzi''. Terry amepata adhabu ya kufungiwa mechi nne na faini ya £220,000 labda kama atakata rufaa juu ya maamuzi ya kosa hilo alilolitenda Oktoba mwaka jana ambalo lilirekodiwa vizuri na kamera za uwanjani. Ferdinand jana alionekana kwatika supermarket mjini Warford huku akilakiwa na mashabiki ikiwa ni mara ya kwanza tangu hukumu dhidi ya Terry ilipotolewa.

No comments:

Post a Comment