Saturday, September 29, 2012

WALCOTT AKIRI KUMMISI VAN PERSIE ARSENAL
Theo Walcott akiwa amebebwa na Van Persie enzi hizo wakiwa wote Arsenal
WINGA wa Arsenal, Theo Walcott amekiri kwamba alijisikia vibaya sana kumuona Robin van Persie akiondoka kwenda Manchester United. 
Walcott amesema alikuwa karibu sana na Mholanzi huyo. 
"Daima unawamisi wachezaji bora na yeye ni rafiki mkubwa na mweledi wa uhakika. Namtakia mema Manchester United. Daima alikuwa akinitafuta na kunisapoti. Nammisi sana lakini unapaswa kusahau na kusonga mbele." alisema Walcott.

No comments:

Post a Comment