Monday, October 1, 2012

THIERY HENRY ABATIZWA KUWA "MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU YA MAREKANI''...NI BAADA YA KUIPAISHA TIMU YAKE YA NEW YORK RED BULLS NA KUSHINDA 4-1


Thiery Henry akishangilia goli
THIERRY HENRY anatajwa kuwa mchezaji bora Marekani mara baada ya kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Toronto.

Mfungaji huyo bora wa zamani wa Arsenal mwenye miaka 35 alifunga goli moja na kusaidia moja kwa moja ufungaji wa magoli mengine matatu.Henry ameshafunga mabao 14 katika michezo 21 msimu huu na amesaidia ufungaji wa mabao 12 kwa timu yake ya Red Bulls.
Bosi wake Henry alisema ''Thiery na wa kipekee.Anatengeneza kila goli isipokuwa lakwake.Anapong'ara namna hii, unaweza kusema ndiye mchezaji bora katika ligi yote''.

No comments:

Post a Comment