Monday, October 1, 2012

CHRISTIANO RONALDO ATAKA KUWEKA REKODI YA KUWA MCHEZAJI WA KWANZA KULIPWA KIASI CHA £400,000 KWA WIKI




Mchezaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anataka kuwa mcheza soka wa kwanza kupokea mshahara wa £400,000 kwa wiki, kwa mujibu chanzo cha habari cha ESPN.

Kutokana na sheria za kodi za Spain  zilivyo, Ronaldo atahitaji kufikia kulipwa mshahara wa £400,000 kwa wiki ili kuweza kupata anachokitaka kuwa mchezaji anayepokea fedha nyingi za mshahara.


Huku akiwa anavivutia vilabu vingi dunaiani, wakiwemo matajiri wa Man City na PSG, mazungumzo ya juu ya hatma ya Ronaldo yapo njiani kuanza.


Ronaldo ametoa taarifa rasmi akisema kwamba 'huzuni' yake aliyosema anayo haihusiani na mambo ya fedha. Lakini chanzo cha habari kilicho karibu na Ronaldo kinasema kwamba Mreno huyo anataka mshahara wake uongezwe mara mbili, na hili litafanya aamini kwamba klabu hiyo ipo tayari kumpigania aendeleee kubaki kwenye klabu hiyo.


Nahodha huyo wa Ureno aliwahi kuwa mchezaji anayelipwa vizuri zaidi duniani wakati akihamia Mafrid mwakak 2009, akiwa analipwa £200,000 kwa wiki, lakini kwa sasa amejikuta ameteremka mpaka kushika nafasi ya kumi duniani, akipitwa na wachezaji kama Samuel Eto'o, Wayne Rooney, Neymar na Didier Drogba pamoja na wengine watano.


Kingine, Madrid kwa sasa wanamiliki asilimia 50 ya haki za picha za Ronaldo, na sasa tayari ameshampita David Beckham kuwa mchezaji ambaye jezi zake zinauzwa sana katika ulimwengu wa soka.


Ronaldo ana mkataba na Madrid unaoishia 2015.

No comments:

Post a Comment